TAARIFA KWA UMMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Ndg. Magesa Mafulu Boniphace anapenda kuwajulisha wananchi wa Sengerema na Watanzania kwa ujumla, juu ya kuibuka kwa wimbi la matapeli ambao wamekuwa wakijitambulisha kuwa ni Maafisa utumishi wa Halmashauri na kuomba fedha watu wenye kusaka ajira za “Maafisa Watendaji wa Vijiji” kwa madai kuwa Mkurugenzi anazo nafasi nyingi za ajira kwa kada husika jambo ambalo halina ukweli wowote.
Kupitia taarifa hii Mkurugenzi anawatahadharisha wananchi kuwa makini na Matapeli hao, na kwamba ofisi ya mkurugenzi haitawajibika kwa lolote. Huku akiwaasa wakazi wa Sengerema kuwa na tabia ya kufika ofisi ya Mkurugenzi(W) ili kupata ufafanuzi wa Mambo mbali mbali na kuacha kuwatumia watu wasio waaminifu katika kupata habari.
Mwisho amewakumbusha wananchi kutoa au kupokea rushwa ni kosa kisheria, Tukumbuke Rushwa ni adui wa haki na maendeleo ya nchi.
Imetolewa:
Sylivanus Mdalami
Afisa Habari
Kitengo cha Tehama na Uhusiano
SENGEREMA
08/01/2018
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.