Idara ya Afya ni moja ya Idara muhimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambayo huwa na jukumu la kusimamia shughuli zote za Afya ndani ya Halmashauri
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema katika utoaji wa huduma bora za Afya inatekeleza majukumu mbalimbali
Wilaya ina jumla ya vituo 6 vya kutolea huduma mbalimbali za afya. Kati ya hivyo vituo vya Afya moja (1) ni Hospital inayomilikiwa na serikali kwa kushirikiana na taasisi ya dini, zahanati 18 zinazomilikiwa na serikali, zahanati 3 zinazomilikiwa na watu binafsi, zahanati 3 Parastatal na kliniki 1 ni maternity home .
IDADI YA WATUMISHI
Idara ina watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo daktari wa meno, Madaktari, Madaktari Wasaidizi, Matabibu, Matabibu Wasaidizi,Maafisa Waaguzi, Maafisa Wauguzi Wasaidizi, Wauguzi, Fundi Sanifu vifaa tiba, Wateknolojia Dawa, Wateknolojia Maabara, Fundi Sanifu umeme, Wahudumu wa Afya, Watunza kumbukumbu,Katibu Mahususi, Walinzi, madereva na kada nyingine
HUDUMA ZA AFYA ZINAZOTOLEWA
Huduma za afya zinazotolewa katika vituo vya kutolea huduma ni pamoja na huduma za Wagonjwa wa nje (OPD) na huduma za Wagonjwa wa ndani au wagonjwa waliolazwa (IPD). Huduma za Wagonjwa na ndani hutolea katika Hospitali ya wilaya na kituo cha Afya cha St.Elizabeth. Huduma zingine zinazotowa ni huduma ya Afya ya mama,baba na mtoto,huduma ya kujifungu huduma ya Afya ya Akili, Kituo cha huduma na tiba cha Ukimwi, Kitengo cha macho.
HUDUMA ZA AFYA KWA MAMA NA MTOTO
Huduma za afya ya Mama na Mtoto zimeendelea kuimarika. Kumekuwa na ongezeko la kiwango cha wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya. Kwa mfano, kwa wastani wanawake wajawazito wanane (8) hadi kumi (10) hujifungua kila siku katika hospitali ya wilaya. Aidha, vifo vya akinamama wajawazito vimepungua kutoka 11/100,000 mwaka 2014 8/100,000 Disemba 2015, 6/100,000 hadi kufikia Juni 2017 vifo viliripotiwa 3/100,000. Sambamba na huduma hizi za akinamama wajawazito, hutolewa pia huduma za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Kumekuwa na ongezeko la wenza wanaowasindikiza akina wajawazito kutoka 6304 2016 hadi 8618 2017 akinamama wajawazito wanaopata huduma hizi.
HUDUMA ZA CHANJO KWA WATOTO
Huduma za chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) hutolewa katika vituo vyote. Kwa mwaka 2016, ukamilifu wa chanjo ulikuwa 92%. Kwa mwaka 2017 ukamilifu wa chanjo ulikuwa 96%. Huduma za ushauri juu ya lishe kwa watoto wadogo pamoja na mambo mengine ya kuzingatia katika makuzi ya mtoto hutolewa kila siku katika kliniki za watoto. Hakuna watoto wenye utapiamlo mkali walioripotiwa kwa kipindi cha hadi Juni 2016.
HUDUMA ZA VVU na UKIMWI
Huduma za VVU na UKIMWI hutolewa katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya na katika baadhi ya zahanati.
Huduma zinazotolewa ni pamoja kutoa dawa za kufubaza virusi vy a Ukimwi, kupima wingi wa damu, CD4,Wingi wa virus kwenye damu(viral load) na ushauri wa lishe kwa wanaotumia dawa. Kwa kipindi cha mwaka 2016, jumla ya wateja 11,563 walipata huduma mbalimbali za VVU na UKIMWI na hadi Juni 2017, jumla ya wateja 18,566 walipata huduma mbalimbali za VVU na UKIMWI.
HUDUMA ZA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA
Ugonjwa wa malaria umeendelea kuongoza katika kusababisha vifo kwa jamii. Idara imeendelea kutoa huduma mbalimbali za kupambana na malaria. Huduma hizo ni pamoja na kugawa vyandarua 250,000 vyenye viatilifu vya muda mrefu. Zoezi hili lilifanyika kwa ushirikiano na Wizara ya Afya. Aidha, idara imendelea kutoa tiba kinga kwa wanawake wajawazito wote wanaohudhuria kliniki. Idara pia imeendelea kuhakikisha kuwa dawa na vitendanishi vinaendelea kuwepo.
UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA
Pamoja na changamoto zilizopo za upatikanaji wa dawa na vitendanishi, kumekuwa na ongezeko upatikanaji wa dawa kwa mwaka 2016/17.
Dawa muhimu na vitendanishi vimekuwepo wakati wote kwa 40%. Kwa mwaka 2016/17 upatikanaji wa dawa na vitendanishi kwa wakati wote ulikuwa 35%
HUDUMA ZA AFYA KWA WAZEE:
Dirisha la Wazee.
Vituo vya Afya hutoa huduma kwa wazee kwa ubora na uangalifu wa ghali ya juu, kutoka na huduma bora kumekuwa na ongezeko la wazee wanaopata huduma mbalimbali katika vituo vya afya kutokana na huduma bora zinazolewa na vituo
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.