Hadi kufikia mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Sengerema imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendelea kwa wananchi wake kwa kiwango cha hali ya juu.
1. Mwaka huu wa fedha 2019/20 halmashauri ya Sengerema ni miongoni mwa halmashauri 27 tu nchini tuliotengewa fedha za kujenga hospitali ya wilaya. Kwa hiyo Sengerema tutakuwa na hospitali 2 za hadhi ya Wilaya (yaani ya Mission na hiyo ya Serikali itakayojengwa).
2. Tumefanikisha ujenzi wa vituo vya afya Kagunga, Katunguru na Kamanga tulichosaidiwa na wafadhili. Na bado mipango inaendelea kwa kata zingine na zahanati kwa kila kijiji. Shukrani sana kwa ushiriki wa wananchi.
3. Barabara za Sengerema - Nyanchenche - Ngoma A na ile ya Sima - Ikoni tumefanikiwa kuzipandisha hadhi, sasa zinahudumiwa na Tanroads hili nalo ni bao la kisigino.
4. Barabara ya Kamanga-Sengerema - Taratibu zote za maandalizi ya awali zimekamilika kuijenga kwa lami. Serikali inajipanga kulipa fidia kwa watakaoathirika na kutangaza tenda ya ujenzi.
5. Maji:
(a) Sengerema mjini tatizo tulishalitatua.
(b) Kwa sasa Serikali, kupitia Mamlaka ya Maji Mza (MWAUWASA) wanashughulikia ununuzi wa mabomba na vifaa vingine kwa ajili ya ujenzi wa busta pale Mission ili kutatua kero ya maji Mission na Kizugwangoma.
(c) MWAUWASA pia anashughulikia ununuzi wa mabomba kwa ajili ya Ibondo kwa Mwarabu na Zanzibar Mwabaluhi.
(d) MWAUWASA pia anasimamia shoo ya mradi wa Nyampande ambapo mkandarasi yupo site.
(e) Hivi karibuni tenda kwa ajili ya kufikisha maji Sima kutoka Sengerema mjini itatangazwa. Shoo hii pia itasimamiwa na MWAUWASA.
(f) MWAUWASA huyo huyo ndiyo anayesimamia mradi wa maji Nyasigu - Lubungo - Ngoma A wanakamilisha taratibu za uhakiki wa kitaalamu kabla ujenzi haujaanza.
(g) Tukikamilisha mradi wa maji Sima, tutaanza mradi wa maji Balatogwa - Tunyenye.
(h) Mradi wa maji kwa kata zote zinazopakana na ziwa Victoria-Kasenyi, Chifunfu, Katunguru, Nyamatongo, Ngoma, Kahumulo, Kasungamile, Busisi, Buyagu na Igalula.
-Dizaini na taratibu zingine za kitaalamu kuhusu maandalizi ya mradi huu zimeishakamilika Serikali inaandaa tenda kwa ajili ya kupata mkandarasi.
(g) Miradi ya visima nayo inaendelea katika baadhi ya maeneo.
(k) Maji Kang'washi na Mwaliga. Tunasubiri fedha zitoke tukamilishe maboresho ya upatikanaji wa maji katika maeneo haya.
6. Umeme - Mkandarasi yupo jimboni anaendelea kwa maeneo ambayo hayajafikiwa, jimbo ni kubwa ila atamaliza tu, tuvumilie.
7. Ukamilishaji wa maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
-Serikali imeahidi kutoa fedha kuyakamilisha, tuvute subra.
8. Ujenzi wa stendi mpya Bukala:
-Halmashauri tunaendelea kukusanya fedha ili tukamilishe ujenzi huu.
9. Tumefanikiwa kujenga sekondari kila kata.
10. Barabara za Sengerema - Nyehunge na Katunguru - Nyamazugo:
Zimo kwenye mpango wa kujengwa kwa lami.
11. Daraja la Kigongo - Busisi
-Tenda imeishatangazwa.
12. Mgodi wa Dhahabu Ngoma:
-Serikali imeahidi kutoa leseni ya uchimbaji kwa mwekezaji ndani ya mwaka huu wa fedha 2019/20.
-Leseni ikitoka ndiyo ujenzi wa mgodi uanze. Kwa hiyo uchimbaji unaweza kuanza mwaka 2021.
13. Fedha za Mfuko wa Jimbo - Huwa tunapata sh 60 milioni tu kwa mwaka. Matumizi yake ni kama tulivyokubaliana katika vikao vya Madiwani lengo ikiwa ni;
- kuimarisha barabara ambazo hazina bajeti ya Tarura.
14. TARURA
-Wanaendelea kujenga barabara kwa kadri ya upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini.
-TARURA pia anawajibika kuongeza mtandao wa lami kwa barabara za mjini Sengerema. Tutashirikiana nao kufanikisha lengo hili.
15. MICHEZO
Baada ya kupunguza kero ya maji na kupata fedha za hospitali mpya ya wilaya, sasa tunaanza kujielekeza kwenye uimarishaji wa michezo na ujenzi wa uwanja wa michezo mjini Sengerema. Tataendelea kuwajulisha hatua kwa hatua.
16. Busisi - Buyagu - Ngoma A road
-Tunaendelea kufuatilia ahadi ya Mhe Rais kuijenga barabara hii kwa lami.
17. Mradi wa maji Buyagu-Kalangalala-Bitoto:
-Uko kwenye hatua za mwisho kukamilika.
18. Chuo Kikuu Buyagu
-Ujenzi wa Chuo Kikuu hiki cha Kilimo Buyagu/Isole unaendelea vizuri kwa ufadhili wa Wakorea.
19.RUZUKU KWA KAYA MASIKINI.
-Halmashaur ya Sengerema kupitia Mfuko Wa Maendeleo ya Jamii(Tasaf)Imetoa ruzuku ya fedha kwa kaya masikini zaidi 6963.Jumla ya Tsh 968,736,000.00
-Wapendwa haya ni baadhi tu ya mambo tuliyofanya na tunayoendelea kuyafanya.
“Anayepuuza apuuze, ila sisi tunasonga mbele”
&
Sengerema ni yetu sote, tuendelee kuijenga kwa pamoja
Julai, 2019
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.