• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

KISIWA CHA LYAKANYASI CHANUFAIKA NA MNARA WA SIMU

Posted on: July 18th, 2024

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (MB) amesema Serikali inatekeleza Mradi wa ujenzi wa Minara 758 unaogharimu zaidi ya Bilioni 200 utakaonufaisha wananchi Milioni 23.6 kupata huduma bora za Mawasiliano ya intaneti, data na simu.


Mhe. Nape amebainisha hayo leo Julai 18, 2024 Wilayani Sengerema alipokua ziarani kukagua Mnara wa mawasiliano katika Kisiwa cha Lyakanyasi huku akibainisha kuwa wilaya hiyo itanufaika kwa kujengewa minara 2 kati ya 17 inayojengwa Mwanza.


"Minara hii inajengwa na makampuni ya simu tena inagharimu fedha nyingi sana zaidi ya Milioni 350 kwa mnara mmoja tena kwenye maeneo ambayo hayana mvuto sana kibiashara na kwakweli makampuni mengine yasingeweza kwenda kuwekeza hivyo ni lazima ilindwe." Mhe. Nnauye.


Vilevile, amewasihi viongozi wa wilaya kusimamia upatikanaji wa maeneo ya kujenga minara hiyo itakayosaidia kukuza uchumi vijijini na akatoa wito kwa taasisi zinazotoa huduma za Umeme na barabara  kufikisha miundombinu hiyo kwa kipaumbele ili kurahisisha utoaji wa huduma bora pamoja usalama.


Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga zaidi ya Tshs. Bilioni 2.4 kwa ajili ya kujenga minara 17 katika kata 16, vijiji 52 na inatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 296, 410 wa wilaya 5 za Magu, Ilemela, Sengerema, Misungwi na Ukerewe.


Akiwasilisha taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) John Dafa amesema hali ya mawasiliano nchini ni ya kuridhisha kwa zaidi ya asilimia 85 (2G, 3G, 4G) na kwa Mwanza huduma zimefika kwa wananchi kwa wastani wa zaidi ya asilimia 95.


Akizungumzia usajili wa laini za simu amesema Mwanza kuna ongezeko la zaidi ya asilimia 42 kutoka mwaka 2022 kwani wananchi 4,803,249 (Machi 2024) wamesajiliwa kutumia laini za simu na kwamba kuna zaidi ya vituo vya redio 26 mkoani humo kwa sasa.


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba amesema hakuna mtanzania atakaa bila huduma za mawasiliano na kwamba siku za nyuma minara 50 ilijengwa kupitia ruzuku ya awali UCSAF kwa zaidi ya Bilioni 6.6 huku wananchi 885, 420 wakinufaika mkoani Mwanza.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO AJIRA-UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA September 16, 2024
  • TANAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SENGEREMA August 07, 2024
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI UANDIKISHAJI NA BVR August 08, 2024
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • SENGEREMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MIKOPO YA MILIONI 362

    March 05, 2025
  • UMOJA WA WANAWAKE SENGEREMA WATOA MISAADA

    March 04, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.