Kamati ya Bunge ya miundombinu imezitaka Kampuni za Mitandao ya Simu nchini kuhakikisha kuwa pale wanapojenga Minara ya Mawasiliono kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapata huduma za kijamii, kwani makampuni hayo yanafanya biashara.
Serikali imetoa Sh5.4bilioni kwa ajili ya kusambaza huduma za mawasiliano Mkoa Mwanza Ili kuisadia jamii kupata masiliano ya uhakika kupitia mitandao ya simu.
Kauli hiyo imetolewa katika ziara ya kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokuwa ilipotembelea mnara wa simu uliojengwa na ubia kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Vodacom uliopo Kijiji cha Nyampande kata ya Nyampande Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.
Justina Mashamba ambaye ni mkurugenzi Mfuko wa Mawasiliano kwa wote amesema kuwa mnnara wa simu wa Vodacom uliojengwa Kijiji cha Nyampande utasaidia wakazi 6000 wa Kijiji hicho kupata mawasiliano ya uhakika huku kati yao 2500 wakipata huduma ya intanert.
" Kwa Mkoa wa Mwanza pekee kuna minara 40 ya mwasiliano inatekelezwa kati ya hiyo 18 imekamilika na 22 Iko katika hatua mbalimbali za kukamilika " amesema ,Mashamba.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya miundombinu Selemani Kakoso ameitaka Serikali itahakikisha inapeleka mawasiliano kwa jamii ya vijijini ambayo inauhitaji mkubwa wa mawasiliano Ili kuwasaidia.
Diwani wa Kata ya Nyampande George Kazungu ameishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi wa Kata hiyo huku akisema kujengwa kwa mnara wa simu wanaishukuru Serikali kwa kujenga mnara umewaondolea adha ya kupata mawasiliano.
Nape Nauye ni Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari amewataka Wananchi kutunza miundombinu ya mawasilioni ili iweze kudumu na kuisaidia jamii kupata mawasiliano ya uhakika.
Amesema wao kama Serikali wataendelea kuboresha miundombinu ya mawasilioni ili kuwafikia wananchi wote hapa nchini
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.