Jumla ya watahiniwa Elfu nane mia nne arobaini na watatu (8,443) watarajia kufanya Mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza .
Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Msingi wa Hamashauri Mwl.Oscar Kapinga wakati akizungumzia maandalizi ya mtihani huo unaotaraji kuanza kufanyika kesho nchini.
Bw. Kapinga amesema kuwa kati ya watahiniwa hao wavulana ni 4,049 na wasichana ni 4,394 hata hivyo amesema mpaka sasa vifaa vyote pamoja na mazingira ya mtihani huo yamekwishamilika.
Aidha Bw. Kapinga amewataka wasimamizi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani pamoja na wazazi kutowarubuni watoto wao kufanya mtihani huo vibaya kwa makusudi ili washindwe kuendelea na elimu ya sekondari hapo badae.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.